Hiii hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana
Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo.Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.
Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).
Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary).
Primary amenorrhea
Hiii hali ya kukosa hedhi inayoweza kumtokea msichana aliye katika umri wa kuvunja ungo na ambayo huweza kuendana na hali ya kukosa mabadiliko ya kubalehe kama vile kuota matiti au nywele za kinena, au msichana anaweza kuwa na mabadiliko ya kubalehe lakini asipate hedhi.
Secondary amenorrhea
Hii hali ya kukosa hedhi inayomtokea mwanamke ambaye si mjamzito, hanyonyeshi, na ambaye hajavuka umri wa kukosa hedhi (menopause) na wala hatumii njia za uzazi wa mpango kama vile sindano au vidonge, na ambaye hapo awali alikuwa akipata hedhi kama kawaida lakini akasimama kwa miezi mitatu au zaidi.
Mwanamke hupataje hedhi?
Ili mwanamke aweze kuwa na mzunguko ulio sahihi wa hedhi, ni lazima matezi yake ya hypothalamus na pituitary pamoja na kiwanda cha kutengeneza mayai ya kike (ovaries) na mji wa mimba (uterus) vifanye kazi zake sawasawa.
Hypothalamus huchochea tezi la pituitary kuzalisha hormone chochezi ya follicle au follicle-stimulating hormone (FSH) pamoja na homoni ya luteinizing (LH). Hizi FSH na LH kwa pamoja huchochea ovaries kuzalisha homoni za estrogen pamoja na progesterone. Kazi za estrogen na progesterone ni kusababisha mabadiliko katika ukuta wa uterus yaani endometrium ikiwepo kupata hedhi. Ili damu ya hedhi iweze kutoka nje, njia ya uzazi ya mwanamke haina budi kuwa huru yaani isiyo na matatizo yeyote yale.
Amenorrhea husababishwa na nini?
Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi
KWA USHAURI WASILIANA NASI TUTAKUSAIDIA KUPITIA SIMU NAMBA
0624 073 681
USISAHAU KUSHARE KUSAIDIA WENGINE PIA USISAHAU KU LIKE PAGE HII ILI USIPITWE NA MAKALA MBALI MBALI KUTOKA KWETU
0624 073 681
USISAHAU KUSHARE KUSAIDIA WENGINE PIA USISAHAU KU LIKE PAGE HII ILI USIPITWE NA MAKALA MBALI MBALI KUTOKA KWETU

Comments
Post a Comment