DALILI ZINAZOAMBATANA NA MWANAMKE KUKOSA HEDHI.
DALILI ZINAZOAMBATANA NA MWANAMKE KUKOSA HEDHI. Napenda nikukumbushe msomaji kuwa kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana na mambo yafuatayo:- • Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, msomaji kama unaona matiti yako au ya mwenzi wako yanatoa maziwa wakati wewe au huyo mwenzi wako si mjamzito na hunyonyeshi tambua kuwa kuna tatizo katika mfumo wako wa uzazi na ni kiashiria cha kukokosa hedhi hivyo hatua za mapema zinapaswa kuchukuliwa. • Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen. Nitoe tahadhari hapa si kila mwenye vinyweleo vingi na ana ndevu basi anakosa hedhi si kweli lakini kama una dalili hizo na unakosa hedhi yako ya kila mwezi ni vema ukawaona matabibu mapema kwa ajili ya kufanyiwa uchungu...